Nenda kwenye kichapishi na uingize menyu ya kusanidi Wi-Fi kwa kufuata moja kati ya mbinu hapa chini kulingana na kichapishi chako.
Chagua .
Chagua Wi-Fi Setup (Usanidi wa Wi-Fi).
Gusa /, Setup (Usanidi), na kisha Wi-Fi Setup (Usanidi wa Wi-Fi).
Chagua Push Button Setup (WPS) (Usanidi wa Kitufe cha Kusukuma (WPS))/ Push Button (WPS) (Kitufe cha Kusukuma (WPS)).
Bonyeza kitufe cha WPS kwenye kipangishi njia kisichotumia waya (eneo la ufikiaji). Kisha bonyeza Proceed (Endelea) au OK (Sawa) kwenye kichapishi.
KUMBUKA: Ikiwa kipangishi njia kisichotumia waya (eneo la ufikiaji) hakina kitufe, wezesha WPS kwa kutumia programu iliyotolewa na kipangishi njia chako kisichotumia waya (eneo la ufikiajia).
Wakati ujumbe wa kukamilisha umeonyeshwa, bonyeza OK (Sawa) ili ukamilishe usanidi wa Wi-Fi.
Bofya kiungo kifuatacho ikiwa usanidi wa Wi-Fi utashindikana.