Bonyeza kitufe cha WPS kwenye kipangishi njia kisichotumia waya (eneo la ufikiaji).
KUMBUKA:
Ikiwa kipangishi njia kisichotumia waya (eneo la ufikiaji) hakina kitufe, wezesha WPS kwa kutumia programu iliyotolewa na kipangishi njia chako kisichotumia waya (eneo la ufikiajia).
Shikilia chini kwenye kichapishi kwa sekunde tatu.
Taa za hali ya Wi-Fi humweka moja baada ya nyingine. Huenda ikachukua dakika chache kwa kichapishi kuunganishwa kwenye mtandao.
Usanidi wa Wi-Fi umekamilika wakati taa zote za hali ya mtandao zinapowaka kama ilivyoonyeshwa katika mfano unaofuata. Taa ya kulia ya hali ya mtandao huzima baada ya dakika tano.
Usanidi wa Wi-Fi umeshindwa ikiwa taa ya kushoto imezimwa na ya kulia inamweka. Bofya kiungo kifuatacho ili kutatua tatizo.