Tekeleza shughuli zifuatazo kwenye paneli dhibiti ndani ya dakika 5.
Uteuzi wa menyu hutofautiana kulingana na modeli ya kichapishi.
Kwa modeli zenye skrini ya kugusa bonyeza ikoni moja kwa moja kwenye skrini ya kichapishi.
Kwa modeli zisizokuwa na skrini ya kugusa tumia vitufe vya vishale ili uchague vipengee. Kisha bonyeza OK (Sawa).
Hakikisha kichapishi kimewashwa na tayari kutumika.
Nenda kwenye kichapishi na uingize menyu ya kusanidi Wi-Fi kwa kufuata moja kati ya mbinu hapa chini kulingana na kichapishi chako.
Chagua .
Chagua Wi-Fi Setup (Usanidi wa Wi-Fi).
Gusa /, Setup (Usanidi), na kisha Wi-Fi Setup (Usanidi wa Wi-Fi).
Chagua Wi-Fi Auto Connect (Muunganisho Oto wa Wi-Fi) na ubonyeze Proceed (Endelea) au OK (Sawa). Kisha fuata maagizo kwenye skrini ya kichapishi.
KUMBUKA:
Ikiwa skrini ya hitilafu imeonyeshwa, bonyeza OK (Sawa) kwenye paneli dhibiti ya kichapishi. Kisha rejea kwenye hatua ya 1 kwenye skrini hii.
Ikiwa skrini ya Set Network Location (Weka Eneo la Mtandao) imeonyeshwa kwenye kompyuta yako, bonyeza Cancel (Ghairi) ili ufunge skrini.